BUKOBA PAMOJA BLOG
Blog hii itakuletea habari na matukio ya kila siku kutoka Mkoa wa Kagera
Friday, October 19, 2012
Waziri ashangaa abiria kulala kwenye sakafu ya kokoto
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk Charles Tizeba akitoa ufafanuzi wa jambo linaloihusu Wizara yake katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera |
Dk Tizeba akisalimiana na baadhi ya Maofisa waliofika kumpokea katika uwanja wa ndege Bukoba |
Baadhi ya wageni walioambatana na Waziri Tizeba wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera |
Phinias Bashaya,Bukoba
NAIBU Waziri wa Uchukuzi Dokta
Charles Tizeba ameshangazwa na hali inayowakabili abiria wa mikoa ya Tabora na Kigoma ambao
hulazimika kulala kwenye sakafu ya kokoto wakati wakisubiri usafiri wa treni.
Alionyesha kukerwa na hali hiyo
alipokuwa katika ziara yake mjini Bukoba mapema wiki hii wakati akizungumzia
uchakavu wa miundombinu ya reli na kulaumu
wahusika kupuuzia suala la ujenzi wa maeneo ya kupumzikia abiria.
“Nilishanga abiria wa Tabora na
Kigoma kulala kwenye sakafu ya kokoto wanaposubiri usafiri wa treni,huwezi
kuamini kuwa hawa ndio abiria wa Kitanzania wa mwaka 2012”alilalama Tizeba
Alihoji iweje Shirika la Reli(TRA)lishindwe kuboresha maeneo ya
kupumzikia abiria na kuwa kwa kushindwa kufanya hivyo baadhi ya abiria hukwepa
kutumia huduma za usafiri zinazotolewa na shirika hilo.
Pia Waziri Dokta Charles Tizeba alisema
kuwa wananchi wanalazimika kutumia usafiri wa mabasi kwa sababu meli na treni havitoe huduma zinazoridhisha,
huku akiubeza usafiri wa mabasi na kuufananisha na majeneza yanayotembea.
Aidha alikagua maeneo mbalimbali
yaliyopo chini ya Wizara yake ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa Bukoba,eneo
la Omukajunguti unapotarajiwa kujengwa uwanja wa ndege wa Kimataifa Wilayani Missenye
na bandari za Kemondo na Bukoba.
Akizungumzia hali mbaya ya vyombo
vya usafiri majini alisema abiria wanakerwa na hali ya uchafu wa meli
zinazosafiri ndani ya Ziwa Victoria na
kuwa abiria wanakimbilia usafiri mwingine kukwepa hali inayowafanya waonekane
kama walioko mahabusu.
Kuhusu Meli ya Mv Lihemba
inayofanya kazi Ziwa Tanganyika alisema itafanyiwa ukarabati mkubwa na
Ujerumani.Meli ya Mv Lihemba inatajwa kuwa kongwe zaidi duniani ikiwa na umri wa miaka mia moja ambayo tangu
mwaka 1913 inaendelea kufanya kazi za kusafirisha abiria na mizigo.
Tuesday, October 16, 2012
Uchaguzi wa CCM wazua balaa Mwanza,wajumbe wapata ajali mbaya
Basi lililopata ajali |
UCHAGUZI wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), nafasi ya Uenyekiti mkoa wa Mwanza umeingia dosari baada ya basi
walilokuwa wamepanda wajumbe kutoka Wilayani ya Kwimba mkoani hapa, kupata
ajali mbaya ambapo wajumbe saba wamejeruhiwa vibaya, na dereva wa basi hilo
amefariki dunia.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Bugongwa jijini Mwanza, Jumanne saa 4:45 asubuhi. Chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa dereva wa gari aina ya fuso alipokuwa akigeuza katikakati ya barabara, ambapo dereva wa basi la Bedui alishindwa aliliparamia fuso hilo.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Bugongwa jijini Mwanza, Jumanne saa 4:45 asubuhi. Chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa dereva wa gari aina ya fuso alipokuwa akigeuza katikakati ya barabara, ambapo dereva wa basi la Bedui alishindwa aliliparamia fuso hilo.
Shija Malado ni shuhuda
aliyenusurika katika ajali hiyo mbaya, alimtaja dereva wa basi hilo lenye namba
za usajili T 853 BRB aliyefariki papo hapo kwa jina moja tu la Mihayo.
“Watu 10 waliopata ajali hiyo saba
kati yao ni madiwani wa wilaya ya Kwimba. Mimi nimeruhusiwa muda mfupi baada ya
kupata matibabu katika hospitali ya Bugando”, alisema Malando.
Habari hii imeandikwa
na Sitta Tumma – Mwanza,
Saturday, October 13, 2012
Breaking News.RPC wa Mwanza Liberatus Barlow auwawa
Marehemu Liberatus Barlow enzi za uhai wake |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Liberatus Barlow ameuawa usiku wa kuamkia leo katika tukio linalohusishwa na
ujambazi.
Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini IGP Said Mwema zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha
dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.
Kwa mujibu wa Mwema tarai jeshi la Polisi limetuma askali wa kupeleleza
maujai hayo na ameomba ushirikinao wa wananchi ili kufanikisha kuwatia mbaroni
wahusika wa mauaji.
Friday, October 12, 2012
RCC ya Kagera yapiga 'stop'mradi wa bilioni kumi na moja
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe |
Phinias Bashaya,Bukoba
KAMATI ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa wa Kagera (RCC)imesitisha
mkataba wa ujenzi wa mradi wa jengo la
ofisi ya Mkuu wa Mkoa utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni kumi na moja na kuagiza yawepo mazungumzo na Serikali kutafuta njia nzuri ya kutekeleza
mradi huo.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mjadara mkali wa wajumbe ambao
baadhi yao ilikiwemo kundi la wabunge wakidai mradi huo ambao hadi unasitishwa
ulikuwa umetumia zaidi ya bilioni moja kuwa ulikuwa ni mzigo kwa kuendelea
kuzalisha madeni.
Walisema kuwa pamoja na lengo zuri la kuwa na ofisi za Mkuu
wa Mkoa katika Kata ya Kahororo mradi huo ulikuwa hautekelezeki kwa sasa na
baadhi kushauri watafutwe wawekezaji watakaoweka vitega uchumi katika jengo
hilo lenye vymba tisini.
Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza alisema Mkoa hauna
uwezo wa kuendeleza mradi huo akidai uamuzi haukuwa sahihi,huku Mbunge wa
Nkenge Ansupter Mshama akipendekeza jengo hilo litumike kwa shughuli za utalii.
“Mlianza vyema lakini huu sio wakati unaofaa kuwa na mradi wa
ofisi ya Mkuu wa Mkoa yenye vyumba tisini,tulifanye jengo la utalii wananchi
hawawezi kuchangia jengo wakati huo ukawataka wachangie zahanati”alisema Mshama
Hata hivyo kundi jingine la wajumbe miongoni mwao akiwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Kashunju Runyogote walitetea
ujenzi wa mradi huo ingawa changamoto ilikuwa ni tatizo la upatikanaji wa fedha
usiokwenda na mipango ya utekelezaji.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nassoro Mnambila aliwaeleza
wajumbe wa kikao hicho kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliutaka Mkoa
utafakari tena kama kuna umuhimu wa kuendelea na mradi huo ilhali Serikali
ikiwa inasuasua kutoa fedha za ujenzi wa ofisi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali
Mstaafu Fabian Massawe alisema wataendelea kufanya mazungumzo na Serikali
kushauriana jinsi ya utekelezaji wa Mradi huo na taarifa itawasilishwa katika
kikao kijacho.
Subscribe to:
Posts (Atom)