Phinias Bashaya,Bukoba
ASKOFU Msaidizi wa
Jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini amewashauri wananchi wa Mkoa wa
Kagera kubadilika na kutobweteka kuwa maendeleo katika Nyanja mbalimbali hayapatikani
bila kuyatolea jasho.
Akichangia katika Mkutano wa wadau wa maendeleo ya Mji wa
Bukoba uliofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Fransis alisema mtu anayetafu
maendeleo hatakiwi kukata tama hata kama anakumbana na vikwazo mbalimbali
katika juhudi zake.
Kiongozi huyo wa kiroho alihusisha kuduma kwa maendeleo ya
mji huo na kile alichokiita kuwa ni siasa mfuniko zilizokwamisha mji huo na
kupongeza jitihada mpya zinazofanyika kuuboresha na kuvutia shughuli za kiuchumi.
“Miaka arobaini iliyopita tumekuwa na siasa mfuniko
zilizofunika akili za watu,naunga mkono jitihada za kuuondoa na sasa tunatakiwa
kusonga mbele,mji umeanza kupanuka na amendeleo lazima uyatolee jasho”alisema
Kilaini
Katika Mkutano huo Meya wa Manispaa ya Bukoba Dokta Anatory
Aman alisema utekelezaji wa miradi mbali iliyoidhinishwa na Manispaa inalenga kuongeza
ajira na kuboresha taswira ya mji huo tofauti na mika mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa Dokta
Aman miradi inayotarajiwa kutekelezwa ambayo pia imepata ufadhili ni pamoja na
ujenzi wa soko jipya,kituo cha mabasi,jingo la kitega uchumi na upimaji wa
viwanja elfu tano katika viunga vya mji wa Bukoba.
Pia Mkutano huo ambao idadi kubwa walikuwa viongozi wa
Madhehebu ya dini walikubaliana kuwahamasisha waumini wao kupitia nyumba za
ibada umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kila mwananchi kufanya
usafi na kupanda miti.
Pia wadau hao walibainisha changamoto mbalimbali
zinazoukabili mji wa Bukoba kuwa ni pamoja na ongezeko kubwa la watu
lisiloendana na uboreshaji wa huduma kama miundombinu ya maji safi na maji
taka.
No comments:
Post a Comment