Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe |
Mgeni Rasmi katika mkutano huo mkuu wa 25 wa mwaka wa KDCU Ltd alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe. Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa KDCU Ltd Bwana Prosper Mulungi aliyetaja madhumuni ya mkutano kuwa ni kuupitiha makisio ya bujeti ya msimu wa mwaka 2012/2013, Kufanya uchaguzi wa viongozi wapya, pia kubaini changamoto zinazokikabili chama hicho na kuzitafutia suluhu ya kudumu.
Akihutubia mkutano huo mgeni rasmi Mhe. Massawe aliwasistiza wananchi wa Wilaya ya Karagwe kujiunga kwa wingi zaidi kwenye vyama vya ushirika ili kujiletea maendendeleo kupia vyama hivyo vya ushirika. Pia aliwashauri chama cha KDCU Ltd kuunda SACCOS ya wakulima ili wapatapo matatizo wapate sehemu ya kukimbilia kukopa na au kuweka fedha zao ili wapate faida zaidi ili kuinua uchumi wao.
Mhe. Massawe pia alitoa msistizo mkubwa juu wakulima na wanachama pia viongozi wa KDCU Ltd na viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi ya kitongoji mpaka wilaya kusimamia usafi wa Kahawa ikidhi viwango vya dunia na kupata bei ya kumridhisha mkulima. ”Wananchi hamjali mnachanganya kahawa yenu na mavi ya mbuzi, mawe na kutokausha vizuri kahawa yenu jambo ambalo linaishusha kahawa yetu thamani katika soko la dunia.” Alisema Mhe. Massawe.
Pia Mhe. Massawe aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kutunga na kuzisimamia sheria ndogondogo (By Lwas) juu ya watu wanaofanya biashara ya magendo ya kahawa. Wanannchi wote walisistizwa kuwa walinzi wakishirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali ili kudhibiti magendo ya kahawa ili serikali iweze kupata mapato na kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Karagwe.
Chama cha KDCU Ltd msimu wa 2011/12 kilifanikiwa kununua tani 4000 badala ya tani 3000 zilizokuwa zimekisiwa, pia KDCU Ltd iliweza kupata faida ya Tshs milioni 340 kwa msimu wa mwaka 2011/12. Msimu mpya ambao unaanza tarehe 01/05/2012 KDCU Ltd inatarajia kununua na kukusanya zaidi ya tani 12000 za kahawa zenye thamani ya Tshs. 14,390,000,000.
Habari na Picha kwa Hisani ya Silvester Raphael-Ofisa Habari wa Mkoa
No comments:
Post a Comment