Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KCU wakiwa katika kutano wao wa kawaida wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine ulipitisha malipo ya pili ya kahawa kwa wakulima |
Meneja Mkuu wa KCU Vedasto Ngaiza(wa kwanza kulia)anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chama hicho John Binunshu wakiwa katika Mkutano uliomalizika wiki iliyopita |
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa Bukoba imetupilia mbali pingamizi lilowekwa la kuzuia kufanyika kwa mkutano mkuu wa chama cha ushirika cha Kagera (KCU 1990) ulioandaliwa kwa ajili ya kuichagua bodi mpya ya wakurugenzi ya chama hicho na kutangaza mapendekezo ya bei mpya ya ununuzi wa kahawa kwa msimu wa mwaka 2012.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Kagera,na kutupilia mbali pingamizi la kuzuia mkutano mkuu utakaofanyika mei 3, mwaka huu lililokuwa limewasilishwa katika mahakama hiyo na Diocress Rutabana na Sued Juma Kagasheki wakisimamiwa na wakili maarufu mkoani Kagera Josephat Rweyemamu.
Rutabana na Kagasheki walikuwa wameweka pingamizi la mkutano huo kwa madai kwamba baadhi ya wawakilishi wa mkutano huo mkuu wa cha hicho sio halali, walikuwa wakidai kuwa kila chama cha msingi kinachounda chama cha ushirika mkoani Kagera kuwa kinapaswa kuwasilishwa na wajumbe wawili wawili na wala sio ya wajumbe watatu toka katika chama cha ushirika.
Mashauri aliiambia mahakama hiyo kuwa pingamizi hilo lililokuwa limewekwa kwamba sio sahihi hivyo aliamuru taratibu za maandalizi ya mkutano mkuu wa chama cha ushirika mkoani Kagera uendelee na akasema kuwa kama walalamikiaji hawaridhiki na maamuzi yaliyotolewa wanaweza kukata rufaa katika ngazi nyingine.
No comments:
Post a Comment