Mkuu Mpya wa Wilaya ya Karagwe Darry Rwegasira akila kiapo cha kutumikia nafasi hiyo leo Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera |
Mkuu wa Wilaya mpya ya Kyerwa Luteni Kanali Mstaafu Benedict Kulikila Kitenga akila kiapo cha kuwa kushika majukumu ya kuongoza wilaya hiyo leo asubuhi |
Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbali mbali ya dini wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Kagera |
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Bukoba Magreth Abuhoro akisalimiana na Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Bwana Fumbuka baada ya kuapishwa kwa wakuu wapya wa Wilaya |
Katika hotuba aliyoitoa mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni,Kanali Masawe amesema ni aibu mkoa wa Kagera kuwa katika nafasi ya 19 kwa kiwango cha umasikini ikilinganishwa na mikoa mingine.
Amewataka kuongeza pato la Mkoa wa Kagera kwa kusimamia shughuli za kilimo chenye tija huku akiwaonya wananchi wanaoendekeza uzurulaji na ulevi badala ya kutumia muda huo katika shughuli za uzalishaji.
Katika sherehe za kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya zilizofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pia Knali Massawe amewataka viongozi na wananchi kutembelea vivutio mbalimbali katika wilaya za Mkoa wa Kagera kama njia ya kuvitangaza.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wakuu wapya wa wilaya walioapishwa,Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Issa Njiku amesema watazingatia maelekezo waliyopewa na kuhaidi kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wengine katika maeneo yao ili kufikia lengo la kurudisha heshima ya Mkoa wa Kagera katika shughuli za kiuchumi na kijamii kama ilivyokuwa baada ya Uhuru.
No comments:
Post a Comment