Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera SSP Peter Matagi akionyesha bunduki aina ya SMG baada ya kumkamata Mshauri wa Mhakama ya Mwanzo Lusahunga akiwa katika harakati za kwenda kufanya uhalifu. |
MSHAURI wa mahakama ya Mwanzo Lusahunga wilayani Biharamulo
Mkoani Kagera Enos Kazikie(43)amekamatwa na bunduki aina ya SMG na risasi 248
akiwa katika safari ya kwenda kufanya uhalifu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Peter
Matagi mtuhumiwa huyo mkazi wa kijiji na Kata ya Nyakanazi alikamatwa tarehe
1,Agosti katika kitongoji cha Kabulaitoke akiwa ameweka silaha hiyo katika buti
ya gari.
Alisema polisi wilayani humo walipata taarifa kuwa katika
kijiji hicho kuna jambazi anamiliki silaha ndipo ufuatlijai ulipofanyika na
mtuhumiwa kunaswa na bundiki na risasi hizo.
Alitaja namba za silaha hiyo kuwa ni SMG 4707,magazine moja
na risasi 248 akisema kiasi cha risasi kilichokamatwa ni kikubwa nakama
zingeendelea kumilikiwa na majambazi
zingehatarisha maisha ya wananchi na mali zao.
Pia Matagi amesema mbali na kuhusishwa na uhalifu mtuhumiwa
huyo inaaminika alikuwa safarini kwenda kuuza siraha hiyo na kuwa msako wa
kuwatafuta majambazi wengine waliokuwa wakishirikiana na mtuhumiwa unaendelea.
“Msako wa kuwatafuta majambazi wengine waliokuwa
wanashirikiana na mtuhumiwa unaendelea,bunduki alikuwa ameiweka kwenye buti ya
gari hata dreva wake gari hilo hakuwa na taarifa”alibainisha Matagi
Kufuatia tukio hilo Kaimu Kamanda Peter Matagi amewataka
wananchi Mkoani Kagera kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama wanapotilia
shaka mienendo ya baadhi ya wananchi wanaotuhumiwa kujihusisha na uhalifu.
No comments:
Post a Comment