Thursday, April 12, 2012

Askofu Kilaini.Tuwaenzi waliotutangulia

Bukoba
ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Cathoric la Bukoba Methodius Kilaini amesema serikali inashindwa kupata mafanikio katika utekelezaji wa mipango mbalimbali kutokana na kupuuzia ushauri na maoni ya wasomi.
Alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kijiji cha Bwegeme kata ya Katoma nje kidogo ya mji wa Bukoba wakati alipohudhuria kumbukumbu ya miaka thelathini ya ya kifo cha Profesa Justinian Rweyemamu aliyekuwa mtaalamu wa uchumi.
Askofu Kilaini alisema mtaalamu huyo aliyefariki mwaka 1982 ni miongoni mwa wasomi wa masuala ya uchumi nchini aliyeonya juu ya athari za serikali kujihusisha na masuala ya biashara kwani isingeweza kupata faida.
"Kuna umuhimu wa kuwaenzi ndugu waliotutangulia, Profesa Justinian Rweyemamu alikuwa mfano na tulijifunza mengi kutoka kwake aliionya serikali isifanye biashara kwani tutafika pabaya"alisema Kilaini katika salamu zake fupi.
Kwa mujibu wa Kilaini nchi nyingi duniani zinatumia vitabu vya masuala ya uchumi alivyoandika na ni miongoni Mtanzania wa kwanza msomi wa uchumi aliyechaguliwa kuwakilisha wasomi wa Afrika kabla ya Uhuru.
Pia wasifu wa mtaalamu huyo unaonyesha kuwa pamoja na kutumikai nafasi nyingi serikalini mwaka 1975 alikuwa Katibu wa kudumu katika Wizara ya Mipango na baadaye msaidizi wa masuala ya uchumi chini ya uongozi wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Nyerere.
Mtaalamu huyo inadaiwa alishauri njia sahihi za kukuza uchumi ambapo aliandika kitabu cha kutoendelea na mapinduzi ya viwanda Tanzania cha mwaka 1973,Ujumbe wa Mwelekeo mpya na kufundisha uchumi katika Afrika.
Awali Padri wa Parokia ya Katoma Donatus Tugatangya aliwaonya wananchi wa Mkoa wa Kagera juu ya kujindaa na changamoto za soko la Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Alitaka wananchi wasinga'ang'anie kulima katika ardhi walipozaliwa kwani ongezeko la watu linafanya isikidhi mahitaji na kuwashauri kuunda vikundi na kuendesha shughuli za kilimo katika wilaya ambazo bado zina ardhi ya kutosha

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini

No comments:

Post a Comment