Monday, April 16, 2012

Kupanda na Kushuka kwa UKUTA

Wajumbe wa Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania(UKUTA)wamemaliza Mkutano wao Mjini Bukoba ambao pamoja na mambo mengine,lilifanyika kongamano la kujadiri mwelekeo wa lugha ya Kiswahili na viashiria vinavyotishia kuiondoa lugha hiyo katika matumizi rasmi.

Hata hivyo ili kuiokoa(UKUTA)wajumbe walihairisha ajenda ya uchaguzi na badala yake kuteua viongozi wa mpito baada ya kubainika mapungufu makubwa katika katiba ya Chama hicho,na hata udhaifu mkubwa uliopo kwa viongozi waliopo.

Safari ya kuiokoa UKUTA ilianza kwa Wajumbe waliopendekezwa na Mkoa kufanya vikao vya maandalizi
Taswira ya UKUTA kwenye vyombo vya Habari
Haikuwa kazi rahisi.Mwenyekiti wa UKUTA Mkoa wa Kagera (kulia)Abdalah Msakanjia akiongoza moja ya kikao cha maandalizi
Hatimaye iliwezekana.Baadhi ya washiriki katika kongamano la kujadiri hatima ya Lugha ya Kiswahili lililofanyika katika ukumbi wa Lina's mjini Bukoba

Nipige Tafu!.Huyu ni mjumbe wa Mkutano wa UKUTA kutoka jijini Dar es salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi baada ya kuhairishwa kwa Mkutano mkuu wa Uchaguzi
Mariamu Ismail'Mama Mipango'akiimba shairi maalmu la kuupongeza Uongozi wa Mkoa wa Kagera kufanikisha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa UKUTA.

Wajumbe katika picha ya kumbukumbu
Mwenyekiti wa Chama Cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Mkoa wa Kagera(UKUTA)Abdalah Msakanjia akimuongoza Mzee Amir Andanenga'Sauti ya Kiza'kutoka nje ya ukumbi.Mzee Andanenga ni mshairi maarufu nchini ambaye alipachikwa jina la Sauti ya Kiza baada ya kupofuka macho mwaka 1975.Mzee Msakanjia pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Muda wa UKUTA Taifa ambapo pamoja na wajumbe wengine watafanya marekebisho ya katiba na kuitisha uchagui Mkuu wa Chama hicho
Wajumbe katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mzee Amir Andanenga kwa jina la Ushairi'Sauri ya Kiza'akifuatilia mjadala wa matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera uliofanyiaka katika Ukumbi wa Lina's mjini Bukoba
Profesa Mugyabuso Mulokozi (katikati)kuttoka Taasisi ya Taalma za Kiswahili chuo Kikuu cha Dar es salaam(TATAKI)akiwa katika picha pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa UKUTA

No comments:

Post a Comment