MKUU wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe amewaasa waandishi wa habari Mkoani hapa kutoa kipaumbele kwa habari za kutangaza maendeleo na fursa mbalimbali zilizopo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo mchana Kanali Massawe amesema habari nyingi za maendeleo hazijatangazwa vya kutosha katika vyombo vingi vya habari kama ilivyo katika Mikoa mingine.
Amesema Mkoa wa Kagera unatekeleza mipango mingi ya maendeleo ambayo haipewi nafasi kubwa na waandishi wa habari na kuwataka pia kuandika habari za kuvutia fursa mbalimbali za uwekezaji.
'Mkoa wetu wa Kagera una ukame wa habari katika vyombo vingi vya habari,tunataka uanze kusikika tangazeni pia mambo yanayoweza kuwaathiri wananchi ili mradi mpate ufafanuzi wa viongozi husika'alisema Massawe
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwakumbusha waandishi wa habari kwenda kwa viongozi sahihi wanaoweza kutoa ufafanuzi wa habari au mambo wanayoyafuatilia kabla ya kuyatangaza au kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Alitumia nafasi hiyo ya kusisitiza kampeini ya usafi inayoendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kuwabaini watu wanaowaachisha wanafunzi wa kike masomo baada ya kuwabebesha ujauzito.
Pia Massawe aliwaonya viongozi wa kisiasa wanaokwamisha utekelezaji wa mambo mbalimbali katika maeneo yao kwa kisingiziio cha kuwatetea wapiga kura wao.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya habari zilizochapishwa katika magazeti hivi karibuni zinazohusu Mkoa wa Kagera |
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa |
Waandishi wa habari wakinukuu mambo muhimu yaliyokuwa yakitolewa ufafanuzi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera |
Mkurugenzi mpya wa Radio Kasibante FM ya mjini Bukoba Richard Leo(kulia)akiwa na Katibu Tawala Msaidizi Richard Kwitega wakati wa Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na waandishi wa habari |
Mkurugenzi wa Radio Vision Fm ya mjini Bukoba(Valerian) akitoa ufafanuzi wa jinsi kituo chake cha Redio kinavyoshiriki mipango mbalimbali za kuhamasisha maendeleo ya Mkoa wa Kagera |
No comments:
Post a Comment