Phinias Bashaya,Karagwe
BAADHI ya wananchi wa Wilaya ya
Karagwe wamewalalamikia maofisa watendaji wa vijiji na kata kwa kuwatoza zaidi
ya shilingi 30,000 kama gharama za kuandikiwa barua za utambulisho kwenda
katika ofisi na taasisi mbalimbali.
Adha hiyo imewakumba zaidi wananchi
wanaohitaji barua za utambulisho kutoka kwa maofisa hao ili waweze kupewa
malipo ya fidia ya kupisha ujenzi wa barabaraya kiwango cha lami kutoka Kyaka
hadi Bugene.
Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya
wananchi ambao tayari wametozwa kiasi hicho cha fedha,walisema huojiwa kwanza
kama wametoa michango ya ujenzi wa shule za sekondari za Kata na Zahanati kabla
ya kunadikiwa barua za utambulisho.
Walisema mwananchi anayeshindwa
kuonyesha stakabadhi za michango mbambali hulazimika kutozwa kuanzia shilingi
elfu thelathini ili aweze kuandikiwa barua ya kumtambulisha ili apewe malipo
yake.
Pia wananchi wanaohitaji barua za
utambulisho kwa ajili ya kuwadhamini ndugu zao katika vituo vya polisi,mahakama
na wanaotaka kufungua akaunti za akiba katika Benki hutakiwa kuonyesha
stakabadhi za michango au kulipa kiasi icho cha fedha vinginevyo hapewi barua
ya utambulisho.
“Hii ni aina mpya ya ufisadi
nimeandikiwa barua ya utambulisho na Mtendaji wa Kata baada ya kulipa kiasi cha
shilingi elfu thelathini nilihitaji kwenda kumdhamini ndugu yangu kituo cha
Polisi”alisema mmoja wa wananchi kutoka Kata ya Bugene.
Baadhi ya wananchi waliolalamika
walikiri kuwa hawajawahi kutoa michango ya shughuli za maendeleo kwa zaidi ya
mwaka huku wakidai kuwa kiasi cha fedha wanayotozwa ni kubwa mno huku
wakionyesha wasiwasi wa matumizi ya fedha hizo pamoja na kuwa wanapewa
stakabadhi za malipo.
Pamoja na walalamikaji kuomba majina
yao yahifadhiwe kwa hofu ya kupata msukosuko baadaye,mmoja wa wakazi wa Kijiji
cha Kishao Justus Daniel alisema utaraibu huo unatumika katika Kata nyingi za
Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bosco Ndunguru alisema suala la kutoza
wananchi fedha kwa ajili ya kuandikiwa barua halipo na kuwataka walalamikaji
wafike ofisini kwake na kumtajia majina ya wahusika ili aweze kuwachukulia
hatua.
Alisema yuko tayari kurudishia fedha
za wananchi endapo watendaji wanaohusika na tuhuma hizo watajulikana na
kuwa ofisi yake iko tayari kuidhinisha barua hizo bila malipo kwani wanalipwa
mshahara kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
No comments:
Post a Comment