Monday, May 14, 2012

Aliyetaka kumng'oa Mwl Nyerere mwaka 1965 haijui katiba ya sasa

Mzee Leopord Rwizandekwe mkazi wa kijiji cha Katendaguro Tarafa ya Kiziba Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera ambaye mwaka 1965 alitaka kumng'oa mwalimu Nyerere kabla ya jina lake kuenguliwa na vikao vya Chama amesema haijui vizuri katiba ya sasa na atatoa maoni yake baada ya kuisoma na kuielewa.

Amesema hata hivyo ndiye alimshauri Mwalimu Nyerere kuanzisha vijiji vya Ujamaa walipokutana Uingereza mwaka 1961 wakati huo akisomea sheria.Mzee Rwizandekwe aliwahi kuwa hakimu wa Mahakama ya Rufani ya Buhaya ambapo mtandao huu umemnasa katika moja ya mitaa ya Mji wa Bukoba akitafuta duka zinapouzwa Katiba za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment