Monday, April 23, 2012

Bei ya viwanja Bukoba karibu na bure!

TANGAZO LA VIWANJA
Manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) imekamilisha upimaji wa viwanja takribani 5,000 katika maeneo  mbalimbali.
HivyoMkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba anawatangazia wananchi  wote kuwa, viwanja 5,000 sasa vitauzwa kwa utaratibu ufuatao:-
1.      Kununua Fomu ya maombi ya kiwanja Tshs. 10,000/=(haitarejeshwa) katika Benki ya Posta tawi la Bukoba tu, ambapo itapaswa kujazwa na kurejeshwa.
2.       Fomu za viwanja zitauzwa kuanzia tarehe 23/04/2012 hadi 22/05/2012.
3.      Muombaji atapaswa kulipa Tshs.200,000 kama dhamana (Security Deposit) ya kupata kiwanja cha makazi na Tshs.500,000 kama kiwanja si makazi au muombaji ni taasis/shirika. Fedha hii itarejeshwa kama muombaji hatafanikiwa kupata kiwanja kupitia Benki ya Posta.
4.       Kila mita ya mraba ya eneo (1M2 ) itauzwa kati ya Tshs.3,000 – 4,500 kwa kutegemea matumizi ya kiwanja na eneo  ambalo kiwanja kipo.
5.       Wale waliotwaliwa maeneo yao kwa ajili ya upimaji viwanja pamoja na wale waliowahi kuchangia gharama za upimaji toka mwaka 2002 nao watapaswa kununua fomu. Punguzo lao maalum la bei litakuwepo wakati wa kuuza kiwanja.
6.       Viwanja vyote vimewekewa barabara na vipo jirani na miundombinu muhimu ya  maji na umeme.
7.       Bei ya kiwanja ni pamoja na kutayarishiwa hati miliki ya kiwanja atakachopewa mnunuzi.


                            Robert Kwela
KAIMU MKURUGENZI WA MANISPAA
BUKOBA.

1 comment:

  1. Poleni na kazi wakubwa,samahani,ninaweza kupata orodha ya bei za viwanja kwa maeneo ya Mugeza na Ihungo?Ni shilingi ngapi kwa mita za mraba?Mungu awabariki sana Wadau.

    ReplyDelete