Thursday, May 10, 2012

Massawe Day katika Kata ya Miembeni

Kila Alhamisi ni siku maalumu ya usafi kwa wakazi wa Mji wa Bukoba.Hapa ni katika Kata ya Miembeni karibu na Kituo Kikuu cha Polisi  mama huyu akiwajibika

Mwandishi wa Tanzania Daima na Mtangazaji wa zamani wa Redio Kasibante Antidius Kalunde akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe na kumpongeza kwa juhudi zake za kusimamia sheria za kuweka mji wa Bukoba katika hali ya usafi

Kijana akipewa kibano baada ya kukutwa katika eneo ambalo halijafanyiwa usafi
Huyu sio ofisa wa Manispaa ya Bukoba bali ni mwandishiwa habari akichungulia katika kitabu cha stakabadhi ya malipo ili kufahamu idadi ya wananchi waliopigwa faini na kiasi cha makusanyo baada ya kukutwa maeneo yao ni machafu.

No comments:

Post a Comment