Monday, April 16, 2012

Wahaya na kinywaji cha Rubisi!

Wahaya kama yalivyo makabila mengine wana kinywaji chao cha asili'RUBISI'ambacho utengenezaji wake huanzia kwenye kifaa maalmu mfano wa mtumbi uliochongwa kwa ustadi kwa kutumia gogo kubwa.

Ndizi zikiwa kwenye kifaa maalmu ikiwa ni hatua za mwanzo za utengenezaji wa Rubisi.Hapa ni katika kijiji cha Ihunga Wilayani Muleba
Ndizi zilizovundikwa huwekwa katika 'mtumbwi' na kukanyagwa kwa miguu hadi hatua ya kupata juisi,ambayo hatimaye huvundikwa kwa siku kadhaa ili kupata uchachu baada ya kuwekewa mtama uliosagwa.

Baada ya siku tatu kinywaji huwa tayari kwa watumiaji.Hawa ni wakazi wa kijiji cha Buhanga Wilayani Muleba wakifurahia kinywaji
Rubisi pia huzalisha ile pombe kali kabisa ambayo ni haramu kwa Serikali na halali kwa wanywaji wenyewe.

Kinywaji kimekolea.Kila mmoja anatoa maelekezo ambapo hata lugha hubadilika kwa kuchanganya maneno mengi ya Kiingereza
Huyu sio kwamba ni mchoyo bali hataki usumbufu wa kelele za wengine
Maisha yanaendelea
Kinywaji cha Rubisi pia hupewa heshima katika sherehe na matukio muhimu ya kijamii.Hapa ni wiki moja iliyopita katika kijiji cha Bwegeme Kata ya Katoma
Wakulima wa migomba Mkoani Kagera miaka ya hivi karibuni wamejikuta katika changamoto kubwa kufuatia kuibuka kwa magonjwa ya migomba,huku wakishindwa kuendana na mabadiliko badala yake kuendekeza kilimo cha mazoea.
Hakuna mashamba mapya yanayofunguliwa badala yake mashamba yale yale yaliyochoka yameendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi. Ongezeko la watu haliendani na shughuli za uzalishaji.
Mkungu wa ndizi ulioathriwa na ugonjwa wa unyanjano
Ugonjwa wa Unyanjano ambao unajulikana kwa kitaalamu kama (Banana Xanthonas Wilt-BXW)umeleta hofu kubwa kwa wakulima wa zao la migomba kutokana na ugonjwa huo kuenea kwa kasi takribani katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera..
Athari za karibuni za ugonjwa wa Unyanjano zinaonekana katika kijiji cha Ihunga Kata ya Kishanda na baadhi ya vijiji katika Kata ya Buganguzi wilayani Muleba.
Moja ya mkungu wa ndizi ulioathiriwa na ugonjwa wa ukungu katika kijiji cha Bushemba,Kata ya Buganguzi wilayani Muleba
Mshauri wa Kilimo wa Mkoa wa Kagera Dionysius Mabugo anasema tangu kugunduliwa kwa ugonjwa katika Kijiji cha Kabale,tarafa ya Izigo wilayani Muleba mwaka 2005,idara yake inaendesha kampeini ya kuthibiti ugonjwa huo.
.

No comments:

Post a Comment