Tuesday, May 8, 2012

Familia 100 katika kisiwa cha Bumbire zahitaji msaada


Safari ya kufika Kisiwa cha Bumbire ndani ya Ziwa Victoria inaanzia mwalo wa Kyamukwikwi wilayani Muleba

Meli ya Mv Mugendi inayofanya safari zake kati ya Visiwa vya Mkoa wa Mwanza na Kagera ikiwa imepaki katika kisiwa cha Bumbire.
MVUA kubwa ya barafu iliyoambatana na upepo mkali imeharibu mashamba na kuezua nyumba nne katika kitongoji cha Kajure kilichopo katika kisiwa cha Bumbire wilayani Muleba Mkoani Kagera

Kwa mujibu wa Menyekiti wa Kitongoji hicho Deogratias Mutebwa mvua hiyo ilinyesha wiki iliyopita kwa zaidi ya saa kumi ambapo mapande makubwa ya barafu yaliharibu mazao ya mihogo,viazi na migomba.

Akihojiwa kwa njia ya simu,Mwenyekiti huyo alisema familia zaidi ya mia moja katika kitongoji hicho zipo katika tishio kubwa la kukumbwa na baa la njaa baada ya mashamba yaliyotegemewa kuharibika kabisa.

Pia alisema nyumba nne ziliezuliwa na upepo huku nyumba nyingine mbili zikisombwa na mkondo wa maji ambao pia uliporomosha mawe makubwa kutoka milimani ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa.


No comments:

Post a Comment