Friday, April 13, 2012

Ashikiliwa kwa ubakaji wa kikongwe!

Kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Pius Mutashubirwa mkazi wa kijiji cha Kihwera Kata ya Kabirizi Wilayani Muleba anatuhumiwa kumbaka kikongwe mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 ambapo hali yake ni mbaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Salewi
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho Angelo Tebuza ukatiri huo umetokea usiku wa kuamkia leo ambapo kikongwe huyo pia amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Henry Salewi amethibitisha tukio hilo na kuwa hivi sasa mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Muleba.Habari zaidi baadaye

 Wazee waheshimiwe.Moja ya Maandamano ya Wazee wa Wilaya ya Muleba katika harakati za kudai haki zao.

No comments:

Post a Comment