Monday, April 16, 2012

WAZO LA LEO.Kutojua Sheria sio Kinga ya Kosa

Wakati wa kilele cha siku ya sheria nchini mwaka jana,Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Bukoba Gad Mjemas alisema Dira ya Mahakama ni kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati ingawa inakabiliwa na changamoto nyingi zinazochangia manung’uniko.

Jengo la Mahakama ya Mwanzo Kyaka Wilayani Missenyi linavyoonekana hadi siku ya jana
Alisema ucheleweshwaji wa utoaji haki unasababisha mlundikano wa kesi ambapo katika kipindi cha mwezi Januari na Desemba mwaka 2010 majaji wawili waliokuwepo waliamua kesi 237 za jinai kati ya 625 zilizokuwepo huku madai zikiwa 96 kati ya 768.

Alikumbusha kuwa majengo ya mahakama za mwanzo yanasikitisha na kutoa mfano wa mahakama za mwanzo katika Wilaya ya Missenyi kuwa hazionyeshi taswira ya eneo linalotumika kwa ajili ya utoaji haki kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment