Sunday, April 15, 2012

Tukumbushane ajali zenye utata Mkoani Kagera hadi tarehe ya leo

Tangu Mwezi February mwaka huu Jeshi la Polisi bado linaendelea kuchunguza sababu za dreva wa gari hili kuonyesha nia ya kutaka kupaki gari lake kwenye sebule ya nyumba ya mtu.Hapa ni barabara ya kengele tatu.
Hawa ni miongoni mwa washangaaji wa ajabu ya dreva kutaka kupaki kwenye sebule.Ajali ilitokea usiku wa muda usiojulikana na hakuna kifo wala majeruhi vilivyotokea.Ili kuepuka kuingia matatani dreva aliyesababisha ajali alikubari kufanya ukarabati wa nyumba
Hii ni ajali  ya gari lililokuwa limebeba bia ambayo ilitokea eneo la  'Barabara Mpya' nje ya Mji wa Bukoba.Mashuhuda wa ajali hiyo ambao wengi walikuwa ni watoto walikuwa wa kwanza kuripoti kwenye masanduku ya bia. 

Bia zilizokuwa kwenye gari hili hazikuweza kusalimika mbele ya wananchi waliokusanyika kutoka maeneo jirani.

Safari ya kuelekea Kisiwa cha Bumbire inayoanzia katika mwalo la 'Kastamu' mjini Bukoba.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi hadi tarehe ya leo abiria kumi wameishapoteza maisha katika ajali za usafiri wa majini.
Unaposafiri majini,uvaaji wa 'LIFE JACKET'ni muhimu kwa ajili ya usalama wa Maisha yako.Abiria katika mwalo wa Kastamu wakivaa majaketi ya kuokolea maisha kabla ya kuanza safairi ya kuelekea visiwa vilivyopo wilaya ya Muleba
Wako tayari kwa safari

Jeuri ya Pesa.Huyu mama anabebwa kwa gharama ya shilingi mia tano na kuingizwa katika boti.Umbali wa kuifikia boti ni chini ya sekunde 60!


No comments:

Post a Comment