Saturday, April 14, 2012

Madiwani wa Wilaya ya Muleba na Mkopo wa Baiskeli

Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba miezi mitatu iliyopita Madiwani walipinga Mkopo wa pikipiki wakisema hauna tofauti na mkopo wa Baiskeli.Leo hoja hiyo imeibuka tena na hitimisho likawa Diwani atakayekuwa tayari afuate taratibu za kujipatia mkopo huo usiozidi milioni mbili.
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage(CCM)akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani leo
Mmoja wa Watumishi wa Benki ya NMB Tawi la Muleba Mjini Paul Kapenegele  akitoa ufafanuzi kwa Madiwani juu ya taratibu na sifa za diwanwani anayestahili  kupatiwa mkopo wa Pikipiki.
Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage(CCM)akichangia hoja ya mikopo kwa Madiwani baada ya Mada iliyowasilishwa na NMB kabla ya kikao rasmi cha kujadiri bajeti hakijaanza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba George Katomelo akisoma makadilio ya bajeti ya Mapato na Matumizi kwa kipindi cha Mwaka 2012/2013.Katika bajeti hiyo jumla ya shilingi bilioni 41 zinatarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo  nguvu za wananchi na ushuru kwa wafanyabiashara.
Msemaji wa Kambi ya Upinzani Julius Lwakyendera (CUF)akisisitiza kutounga mkono bajeti iliyowasilishwa kuwa inalenga kuwakamua wananchi baada ya kupendekeza  kuanzisha vyanzo vipya vya mapato alivuyosema vitakuwa kero,badala yake alitaka vyanzo vilivyopo viboreshwe na kuthibiti watendaji wsio waaminifu.
Katibu wa Madiwani wa CCM katika Baraza la Madiwani wa Muleba Danstan Mutagahywa akinukuu mambo muhimu wakati Msemaji wa kambi ya Upinzani alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi yake kuhusu Bajeti iliyosomwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Olva Vavunge akitoa ufafanuzi kwa mambo mbalimbali yaliyohojiwa na madiwani katika bajeti iliyosomwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Hawa nao wanaweza.Huu ndiyo uzuri wa kupitia viti maalmu hulazimiki kuhangaika sana na kero za wapigakura kwani hakuna aliyewapigia kura.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba wakifuatilia kwa makini hoja na mijadara iliyokuwa ikiendelea katika kikao cha leo

No comments:

Post a Comment